Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 26, 2010

PST WAPEWA ULINGO MPYA WA KUHAMASISHA NGUMI


Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania PST, imepokea msaada wa vifaa vya mchezo wa masumbwi vyenye thamani ya shilingi milioni nane kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huo hapa nchini.
Akipokea msaada huo kutoka kwa kampuni ya Bold aviation rais wa PST, Emmanuel Mlundwa amesema vifaa hivyo vimekuja muda muafaka na vitasaidia kurejesha hadhi ya mchezo wa ngumi.

Naye mkurugenzi wa kampuni ya BOLD Aviation John Ndunguru amesema wamevutiwa na vipaji katika mchezo wa masumbwi na kwa kutoa misaada hiyo itasaidia kuwaendeleza na kuwavutia vijana wengi katika mchezo wa masumbwi.
Vifaa vilivyotolewa ni kwa ajili ya utengenezaji wa ulingo wa kisasa wa masumbi na hivyo hii itakuwa suluhisho la baadhi ya mapambano kuchezo sehemu zisizostahili

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...