Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 23, 2010

MAJIRA NA DAR LEO YADHAMINI UZINDUZI WA FIVE STARS


KAMPUNI ya Business Times Limited (BTL), kupitia magazeti yake ya Majira na Dar Leo, yamedhamini uzinduzi wa albamu mbili za bendi ya taarab ya Five Stars Modern utakaofanyika New Msasani Club Oktoba 29, mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa kundi hilo, Hamis Slim, alisema maandalizi ya uzinduzi huo yamekamilika na wasanii wao wako kambini.

¡°Tumejiandaa vizuri kwa uzinduzi wa albamu zetu mbili, tuna imani zitapendwa na mashabiki wa muziki huu kama ilivyokuwa albamu yetu ya kwanza ya Riziki Mwanzo wa Chuki.

Five Stars wanatamba na kibao cha Nichumu, ambacho kimeimbwa kwa ustadi na Issa Kijoti huku kinanda kikipapaswa na Rais wa kundi hilo, Ally Juma 'Ally J'.

Alizitaja albamu hizo ni Shukrani Mpenzi na Ndio Basi tena, ambapo baadhi ya nyimbo zilianza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni.


Slim amesema katika uzinduzi huo kiingilio kimepangwa kuwa sh. 7,000 ili mashabiki wa muziki wa taarab waweze kushuhudia kwa wingi.

Amesema nyimbo za albamu hizo zitatangazwa baadaye ingawa nyingine tayari zimeanza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...