Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 16, 2010

KLITSCHKO KUTETEA TAJI LAKE DESEMBA 11


Klitschko kutetea taji lake dhidi Chisora

BERLIN,Ujeumani

BONDIA Wladimir Klitschko anatarajia kupanda ulingoni kutetea taji lake la ungwa wa ngumi za uzani wa juu unaotambuliwana Shirikisho la Masumbwi la Kimataifa IBF dhidi ya bondia Dereck Chisora litakalofanyika Desemba 11 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mannheim nchini England.Akizungumzia pambano hilo,Klitschko alisema kuwa bingwa huyo wa Jumuiya ya Madola ni mpinzani ambaye anamuhofia.

"Chisora ni bingwa wa Commonwealth ambaye ni mpinzani wangu hatari,"alisema Klitschko. “Chisora ni kijana ,mwepezi na mwenye masumbwi makali,"aliongeza.

Mwezi uliopita,Klitschko alimsimamisha bondia Samuel Peter wa Nigeria katika raundi ya 10 na kufanikiwa kutetea ubingwa wake huo.

Bondia huyo mwernye umri wa miaka 34 raia wa Ukraini vilevilendiye anayeshikilia mikatanda inayotambuliwa na WBO na IBO.

Pambano hilo linadaiwa kuwa ni wakati wa Klitschko kutetea ubingwa mara tisa na kuongeza rekodi ya kushinda mapambano 55-3 wakati kwa . Chisora litakuwa ni la kumfanya kushinda mapambano yote 14 tangu ajitose kwenye ngumi za kulipwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...