Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 21, 2010

MAMA MZAZI WA MUHIGIZAJI ASEMA MTOTO WAKE HUWA ANAMTOROKA


MAMA Mzazi wa staa wa maigizo Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila (pichani) amekiri kupata wakati mgumu kumlea mwanaye kiasi cha kukosa usingizi.

Lucresia alisema katika ‘one on one’ na paparazi wetu Jumapili iliyopita kuwa mwanaye anamshinda ujanja, kwani mara nyingi huwa anamwambia anakwenda kwa rafiki zake lakini baadaye inakuja kugundulika kinyume chake.Alisema, magazeti ndiyo humgutusha na kubaini kwamba kumbe mwanaye alimdanganya.
“Anaweza kuniambia anakwenda kwa rafiki yake lakini baadaye nakuja kuona picha gazetini kumbe alikuwa klabu, inanisikitisha hasa kwa sababu nampenda mwanangu,” alisema Lucresia.

Aliendelea kusema kuwa Lulu akiwa nyumbani ni mtoto mzuri, kwahiyo hata habari za kulewa ameziona kwenye gazeti.

Mama huyo aliongeza kuwa havutiwi na skendo za mara kwa mara kuhusu mwanaye, hasa ya ulevi na vitendo vingine vinavyokwenda kinyume na maadili kwenye jamii.Lucresia alisema: “Mara nyingi matukio ya Lulu yanatokea nikiwa safarini, ananipigia simu na kuniambia anakwenda kwa rafiki yake au sehemu yoyote inayokubalika lakini baadaye nasikia tofauti gazetini.

“Ananidanganya, lakini mimi nampenda mwanangu, napenda awe mtu safi kwenye jamii, azidi kufanikiwa kwa kipaji chake, kwahiyo nikiona jambo baya huwa namkanya.”

Aliendelea kusema: “Unadhani kama mtu anakuaga anakwenda kwenye kazi zake za filamu halafu unakuja kuona tofauti utafanya nini? Kwahiyo mimi huwa namkanya ili awe mtoto bora.”Mbali na kauli hiyo, Mama Lulu pia alipiga picha mbalimbali na mwanaye, huku akimkumbatia, hivyo kusherehesha kauli yake kuwa anampenda na ataendelea kumlea katika misingi bora.

1 comment:

  1. mh pole mama jitaid ipo siku atabadilika tuu,mungu awe nawe katika malezi ya mwanao

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...