Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 12, 2010

KESSY YA JELLY MURO YAKWAMA KUSIKILIZWA 9 MWEZI UJAO


Kesi ya kuomba rushwa ya sh. milioni 10, inayomkabili mtangazaji wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC1), Bw. Jerry Muro na wenzake wawili imekwama kusikilizwa kutokana na wakili wa serikali, Boniface Stanlaus kufiwa na dada yake. Kesi hiyo ambayo ilikuja jana katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kwa ajili ya kuendelea kusikiliza mashahidi wa upande wa mashtaka, ilibid kuahirishwa kutokana na taarifa hizo za msiba.

Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Mkazi anayesikiliza kesi hiyo Bw. Gabriel Mirumbe aliwataka mawakili upande wa utetezi kukuheshimu habari za msiba, na hivyo kukubaliana kupanga tarehe nyingine ya kusikiliza. Hata hivyo aliuonya upande wa mashtaka kuhakikisha unaondoa vikwazo vya kuahirisha kesi hiyo kila siku, kwa madai kuwa hapendi ikae muda mrefu.
"Sitaki kukaa na kesi hii muda mrefu, safari hii nitakuwa mkali sitaku kuahirisha mara kwa mara,"alisema hakimu huyo.

Pamoja na hayo aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 9 mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa tena.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na Bw. Edmund Kapama na Bw. Deogratius Mgassa ambao wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa mnamo Januari 29 mwaka huu, jijini Dar es Salaam wali kula njama ya kula rushwa, kuomba rushwa ya sh. milioni 10 kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bw.Michael Wage na kujifanya maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...