Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 26, 2010

MTUMISHI WA MUNGU ATOA ONYO


MTUMISHI wa Mungu Bw.Innocent Bilakwate amesema ujumbe aliopewa na Mungu juu ya uchaguzi wa Tanzania usipowekewa maanani maafa makubwa yatatokea.

Alisema hayo jana jijini Dar as Saalam kuwa endapo watanzania hawatautilia maanani ujumbe huo na kuombea Nchi amani tuliyonayo itatoweka.

Bw. Bilakwate alisema Mungu amemwonyesha kuwa kuna watu katika vyama vya siasa wanaoshawishi wananchi kuwa tayari kumwaga damu kama njia ya kuingia madarakani, kuleta vujo katika vituo vya kupia kura,kukataa matokeo,kuwatangaza wagombea wanaowataka wenyewe na kuvishambulia vyombo vya usalama.

Alisisitiza kuwa mungu anamjua kiongozi anayewafaa watanzania

Aliongeza kuwa mungu ansema serikali ya Tanzania haina dini na ole wao wanaopeleka siasa kwenye madhehebu yao na kusisitiza kuwa iwapo watakiuka aguzo la mungu upo uwezekano mkubwa wa damu kumwagika

1 comment:

  1. Huyu Jamaa nina dhu amepiga tiki taka ya mbele

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...