Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 29, 2011

AUNT EZEKIEL AADHIMISHA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA WATOTO YATIMA PAMOJA NA WASANII WENZAKE LUKUKI


Aunt Ezekieli akikata keki yake ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaamwa leo.Pembeni ni watoto Yatima wa kituo cha Umra cha Jijini Dar es Salam
MSANII wa Luninga,Aunt Ezekiel aadhimisha siku yake ya kuzaliwa na Watoto Yatima pamoja na Wasanii wenzake lukuki katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salam jana.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili alisema ameamua kuiadhimisha kwa staili hii kwa kujumuika na badhi ya Watoto Yatima wa kituo cha Umri kilichopo Kawe Jijini Dar es Salam kwasababu yeye alitoka katika mazingira hayo mpaka kufikia hapo alipo, hivyo hujisikia furaha kujumuika na watoto yatima mahali popote anapokuwa haswa wakati wa furaha kama siku yake ya kuzaliwa, alisema Aunt Ezekiel.
Aunt Ezekiel katika sherehe hiyo alitimiza miaka 30 hivyo pia aliwahusisha wasanii wenzake mbalimbali kama JB,Dr.Cheni,Mboto,Wema,Cloud,Sinta,Chilele,na wengine wengi pamoja na marafiki zake ambao kila mmoja aliingia viwanja vya Leaders kwa staili yake haswa kwa kuonyesha umarufu wao kwa kumiliki gari la kifahari kila mmoja.
Aunt Ezekiel alizaliw JIJINI Mwanza na alilelewa katika mazingira ya watoto Yatima na katika sherehe yake aliwazawadia watoto Yatima vifaa vya Shule kwa kila mmoja na Chakula kwa Kituo chao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...