Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, October 9, 2011

BALOZI MUTINDA MUTISO AFUNGUA MASHINDANO YA KENYA AIRWAYS GOLF SAFARI


Balozi wa Kenya nchini Tanzania Matiso Mutinda akipiga mpira wa Gofu wakati alipozindua Mashindano ya Kenya Airways Golf Safari kwenye viwanja vya Gymkana jijini Dar es salaam leo huku Meneja mkazi wa Kenya Airways Lucy Malu wa tatu kutoka kulia akishuhudia, mashindano haya yanafanyika nchi zaote za Afrika ambazo kampuni hiyo ina matawi, na mwakani washindi wote kutoka nchi 35 za Afrika watakutana pamoja mwakani na kushindana Nairobi nchini Kenya, ambapo mshindi wa kila nchi wa shindano hilo atagharamiwa kila kitu ikiwa ni pamoja na malazi kwenda kwenye mashindano hayo makubwa nchini Kenya.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mutindo Mutiso kulia akizungumza na Lucy Malu Meneja mkazi wa kampuni ya Kenya Airways wakati wa uzinfuzi wa mashindano ya Kenya Airways Golf Safari.
Meneja mkzi wa Kampuni ya ndege ya Kenya Airways Lucy Malu akiwa katika picha ya pamoja na Mchezaji wa gofu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Aerengeti Breweriers SBL wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Gofu yanayoitwa Kenya Airways Safari Golf yanayozinduliwa leo katika viwanja vya Gymkana jijini Dar es salaam.
Mchezaji wa gofu Mustafa Jacks akipiga mpira wakati wa mashindano hayo yanayoendelea kwenye viwanja vya Gymkana.
Mchezaji K. Mbaya raiwa wa Kenya akipiga mpira katika mzunguko wa kwanza wa mchezo huo.
Victor Joseph akipiga mpira.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...