Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 29, 2011

MBWANA MATUMLA NA FRANCIS MIYAYUSHO WAPIMA UZITO LEO

Mabondia Mbwana Matumla 'Golden Boy' na Francis Miyayusho 'Chichi Mawe' leo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa Ubingwa utakaofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es salaam kesho jumapili OKCTOBA 30.

wakizungumza wachezaji hawo kwa wakati tofauti baada ya kupima wamesema wapo tayari kuonesha mchezo mzuri wa ngumi na kuwapa raha zisizo na kifani kwa sababu akuna kisingizio chochote kile kwa kua tumejiandaa vya kutosha

Licha ya mabondia hawo kupima uzito pia wamepima vipimo mbalimbali ususani Ukimwi, Mkojo kwa ajili ya kuangalia kama mabondia hao kama wanatumia madawa ya kuongeza nguvu.

Pambano hilo kubwa litakuwa la 12 la uzito wa Bantam, ambapo kabla ya mpambano kutakua na mapambano mengine ya utangulizi.

Mapambano hayo ya kati ya Juma Fundi na Fadshili Majia, Mohamed Matumla na Ramadhani Mashudu, Issa Sewe atazidunda na Ramadhani Shauli wakati kwa upande wa ngumi za wanawake Asha Nzowa (Asha Ngedere) atazichapa na Salma Kihobwa (mwajuma Ndalandefu)

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinbu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, MOhamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D;

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...