Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 7, 2011

SHIRIKA LA NDEGE LA KENYA WADHAMINI MICHUANO YA SIKU MOJA YA GOFU


Kapteni wa Klabu ya Gofu (Gymkhana Club Dra es Salaam) Joseph Tango Kulia akiwa na Meneja wa Shirika la Ndege la Kenya Ms.Lucie Malu , wakizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mchana katika ukumbi wa mikutano Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam.
SHIRIKA la Ndege la Kenya jana limetangaza kutoa udhamini mnono katika michuano ya siku moja ya Gofu itakayofahamika kama KQ Golf Safari itakayochezwa katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana Meneja wa Shirika la Ndege la Kenya Lucie Malu alisema wao kama wadhamini wanajisikia furaha kubwa kutoa udhamini kwa wachezaji wa Gofu nchini Tanzania pia ameahidi washindi wawili watapata nafasi ya kwenda Nairobi Kenya ambako watashiriki katika fainali ya michuano hiyo iliyopangwa kufanyika Februari 2012 watakakochuana na washindi waliopatikana katika nchi zingine.

Lucie alisema shindano hilo litakalofanyika Jumamosi (Kesho) ni la siku moja ambapo litachezwa na wachezaji 100 katika mtindo wa Stable Ford yaani watacheza wanne wanne.

Lucie anasema udhamini huo ni wa kipindi cha mwaka 2011/2012 ambapo pia utajumuisha mashindano 35 ambayo yatachezwa katika nchi17 barani Afrika .

Anazitaja baadhi ya nchi hizo kuwa ni pamoja na pamoja Egypt, Cameroon , Afrika ya Kati, Accra Ghana, Cot d’Ivore na Senegal (Afrika Magharibi).

Aidha anazitaja nchi zilizopo katika ukanda wa Afrika Kusini ambapo mashindano ya KQ yatafanyika kuwa ni pamoja na Botswana, Zambia, Zimbabwe, Malawi na Afrika Kusini pia michuano kama hiyo itafanyika katika visiwa vya Shelisheli.

Huku akimalizia katika ukanda wa Afrika Mashariki michuano ya KQ itafanyika Kenya,Uganda na Tanzania.
Wakati huohuo Lucie alisema kwamba kutakuwa na michuano mingine ya KQ itafanyika nje ya bara la Afrika katika miji ya Bangkok , Thailand na Guangzou China.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...