Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 11, 2011

TASWA YAWASHUKURU WALIOFANIKISHA MAFUNZO YA WAANDISHI WA HABARI MOROGOROTASWA imetoa shukurani kwa wote waliofanikisha mafunzo ya waandishi wa habari za michezo yaliyofanyika Oktoba 1 na 2 mwaka huu mkoani Morogoro na kushirikisha wadau 40.Katibu wa TASWA Amir Mhando amewashukuru TASWA Morogoro chini ya uenyekiti wa Nickson Mkilanya kwa ushirikiano mkubwa uliowezesha kufanikisha mafunzo hayo.Pia TASWA inawashukuru wadau wake mhariri mkongwe Said Salim, mdau Anna Kibira, mwanasheria Damas Ndumbaro, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na Alfred Selengia ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya kuendeleza mpira wa wavu Tanzania kwa mada zao walizotoa kwenye mafunzo hayo.Pia tunaishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, pamoja na Kampuni ya mabasi ya Al Saedy kwa kudhamini mafunzo hayo, tunaomba ushirikiano huo uendelee.

Juhudi zinaendelea ili kuhakikisha mafunzo yaliyopangwa kufanyika mkoani Arusha Novemba mwaka huu yanatimia kama ilivyopangwa, tunaamini hakuna lisilowezekana

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...