Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 14, 2011

Mark Allen awapongeza wanamuziki mabalozi wa Malaria nchini


WASANII wa muziki wa kizazi kipya ambao ni mabalozi wa kujitolea wa ugonjwa wa Malaria kwa hapa nchini wamepongezwa na kutakiwa kuendelea na moyo huo wa kujitolea.

Wito huo ulitolewa jana na Mark Allen Mkurugenzi wa Mradi wa Malaria No More kutoka makao makuu ya mradi huo chini Marekani,

wakati wa hafla ya kuwapongeza wasanii hao wanaoendelea na juhudi hizo za kujitolea katika kuhamasisha vita dhidi ya Malaria

.

Alisema kuwa wasanii wa Bongo Flava wa hapa nchini ni mfano wa kuigwa kwa kusaidia jamii kwa kuwa wanafanya kazi hizo bila ya kuweka mbele maslahi yao binafsi.

Mark Allen alisema kuwa wasanii wa nchi nyingine kama Nigeria na Ghana wamekuwa wakiweka mbele zaidi maslahi yao kuliko kutumia majina yao katika kusaidia jamii inayowazunguka.

Allen alisema kuwa kitendo cha wasanii wa fani mbalimbali wa hapa nchini kufanya kazi za uhamasishaji bila ya kuweka mbele hela ni mfano wa

kuigwa na inatakiwa wasanii wote wa hapa nchini kufahamu kuwa mchango wao unaonekana kimataifa.

“ Nimekuwa nikifuatilia nyimbo zenu na vile ambavyo mmekuwa mbele katika kuongeza hamasa kwa wananchi juu ya kudhibiti ugonjwa huu hatari, ni mfano mzuri na pia mnaweza hata kufika mbali kimuziki kwa kusaidia masuala kama haya ya kijamii.” alisema Allen.

Naye msanii mahiri wa muziki wa Hip Hop hapa nchini Joseph Haule (Profesa J) aliomba wadau wa malaria kuwashirikisha kikamilifu mabalozi hao.

Profesa J alisema kuwa mabalozi wamekuwa wakiishia kuhamaisha katika maeneo ya mjini zaidi na kushindwa kufika katika vijiji vya ndani ambapo kuna waathirika wakubwa wa ugonjwa huo.

Profesa J alisema kuwa wao wasanii wakiwa kama mabalozi wanatakiwa kupewa vyandarua vingi pamoja na mafulana yenye ujumbe wa Malaria ili waweze kushiriki kikamilifu katika uhamasishaji.

Wasanii walio wengi walioshiriki katika hafla hiyo walionekana kuguswa zaidi na namna ambavyo wanashirikishwa katika mapambano hayo ambapo wengi walisisitiza zaidi suala la upatikanaji wa mrejesho wa kazi za uhamasishaji wanazozifanya.

Naye Meneja wa mradi wa kupambana na Malaria wa Zinduka, Sadaka Gandi, alisisitiza ushirikiano kati ya wadau wa Malaria kama vile PSI, na Shirika la Msalaba Mwekundu, Red Cross katika kufanya tafiti za pamoja kuhusiana na ugonjwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...