Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 5, 2011

Martinez amtwanga Barker kwa KO


Martinez amtwanga Barker kwa KO


Atlantic City, Marekani

DHAMIRA ya Darren Barker kuishutua dunia imeingia dosari baada ya kutwangwa kwa KO katika raundi ya 11 na Sergio Martinez.


Barker mwenye miaka 29, aliahidi kurejea

Atlantic City akiwa na mkanda wa dunia wa wa WBC uzani wa middle uliokuwa ukishukiliwa na Martinez.


Lakini upiganaji wake mzuri katika ukumbi wa Boardwalk uliishwa baada ya kutwangwa ngumi ya nyuma ya sikio.


Bingwa huyo wa Ulaya alishindwa kuamka na kuendelea na pambano wakati refa

Eddie Cotton akimhesabia hadi 10 wakati zimbakia sekunde 91 katika raundi hiyo.


Akiwa na maumivu Barker alisema: "Sikumbuki ngumi (iliyompiga), miguu yangu ilianguka chini yangu.


"Nilikuwa nikijaribu kusimama lakini sikuweza.Nimesikitishwa kwa kuwa ilikuwa imebaki raundi moja na nusu tu iliyokuwa imebaki.


"Nilikuwa nikijisikia vizuri pale na sikuhisi kuwa kulikuwa na ngumu nzito kabl ya ile.


"Nilikamatwa na kitu na miguu yangu ilikosa nguvu. Kweli nimesikitishwa kamba sikuweza kuuleta ubingwa nyumbani."Barker alikwenda katika mechi hiyo huku akiwa hajapoteza pambano katika mechi 23 ambapo alitwaa ubingwa wa Uingereza, Jumuiya ya Madola na Ulaya.


Alikwua hapewi nafasi ya kushinda mbe ya macho ya watu wengi, lakini alikuwa kwenye tabu katika raundi ya 10 dhidi ya mtu ambaye yuko katika namba tatu kwenye viwango vya Dunia.


Lakini mpiganaji huyo wa London ameondoka Marekani akwia kichwa juu kutokana na upiganaji wake mzuri.


Amemwacha Martinez akiwa anatiokw ana damu puani na mpiganaji huyo wa Argentina alimsifu mpinzani waka kwa kumpa kazi ya kufanya kabla ya kuibuka na ushindi.Bonsi huyo mwenye miaka 36 anayepigana kwa mkono wa kushoto alisema: "Sikuchanganyikiwa hata kidogo, ilikuwa ni kazi nzuri ya Barker.


"Nilitakwia kuyapooza mashambulizi yake, nilitakiwa kumwangusha chini."


Martinez, ambaye hakutaka kukanusua uwezekanow akupigana na Floyd Mayweather, aliongeza : "Nilijua kuwa pambano hili lingekuwa kama hivi.


"Nilipanga hili na kiwa wakati kupata upepo wa pili. Tulifanya mzoezi kwa hili, ni sehemu ya mpango wetu unavyokwenda.


"Tulijua kuwa tutapata uimara kadiri pambano linavyokwenda. Nilikuwa nikiendelea kurusha ngumi ya kulia kwa sababu nilikuwa nikijua haraka au baadaye nitaanda kumpata."

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...