Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 15, 2011

MAKAMU WA RAIS AWASHA MWENGE WA UHURU NA BUTIAMA SIKU MAALUM YA KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa mbio za mwenge huo mwaka 2011- 2012 Mtumwa Rashid Halfan, kutoka mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa ajili ya kuanza mbio za kukimbiza katika mikoa yote ya Tanzania baada ya kuuwasha rasmi leo katika kijiji cha Butiama Mkoani Mara.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la mauwa kwenye Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalim Julius Nyerere baada ya misa maalum ya kumkumbuka muasisi huyo wa Taifa la Tanzania iliyofanyika leo kijijini kwake Mwitongo Butiama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza iliyoambatana na maadhimisho ya miaka 50 Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika jana katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mara. Kushoto ni, Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Dkt Emanuel Nchimbi
Muandishi wa Habari wa Idara ya Habari Maelezo, Anna Itenda, akiweka shada la mauwa katika kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalim Julius Nyerere kwa niaba ya waandishi wa habari wa Tanzania wakati wa misa maalum ya kumkumbuka muasisi wa Taifa la Tanzania iliyofanyika jleo kijijini kwake Mwintongo Butiama.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...