Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 7, 2011

TBL YAKABIDHI MRADI WA MAJI WA MIL 21 SOKO LA MACHINGA MCHIKICHINI


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto) akifungulia maji wakati wa uzinduzi wa mradi huo, ambao ulikabidhiwa kwa uongozi wa Soko la Machinga. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa TBL, Steve Kilindo ambayo imejenga mradi huo kwa sh. mil. 21.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kulia), Mkurugenzi wa Uhusiano wa TBL, Steve Kilindo (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu wakiwa na furaha baada ya kukabidhi mradi huo wa maji kwa uongozi wa Soko la Machinga la Mchikichini, Ilala, Dar es Salaam
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto) akimtwisha mfanyabiashara wa Soko la Machinga la Mchikichini, Asumpta Mosha ndoo ya maji baada ya kuzindua mradi wa maji uliojengwa kwa sh. mil. 21 na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Hafla hiyo ilifanyika sokoni hapo Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...