Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 5, 2011

Kamati ya mashindano TFF kujadili Daraja la Kwanza Oktoba 10


Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), litakuwa na kikao na viongozi wa klabu 18 za Ligi Daraja la Kwanza Oktoba 10, mwaka huu.

Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, amesema ligi hiyo itakayoanza Oktoba 15, mwaka huu, itashirikisha timu za AFC ya Arusha, Burkina Faso ya Morogoro, Majimaji ya Ruvuma, Mbeya City Council ya Mbeya, Mgambo Shooting ya Tanga, Mlale JKT ya Ruvuma na Morani ya Manyara.

timu nyingine ni Polisi ya Dar es Salaam, Polisi ya Iringa, Polisi ya Morogoro, Polisi ya Tabora, Rhino Rangers ya Tabora, Samaria ya Singida, Small Kids ya Rukwa, Tanzania Prisons ya Mbeya, Temeke United ya Dar es Salaam na Transit Camp ya Dar es Salaam, ambazo zitawekwa katika makundi matatu.

Wambura amesema timu za Majimaji na Small Kids, mpaka sasa hazijalipa ada ya ushiriki ya sh. 200,000 na kwamba, zimetakiwa kulipa ada hiyo kabla ya Oktoba 10, mwaka huu ambayo ndiyo siku ya kupanga ratiba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...