Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 13, 2011

Tanzania Distilleries yapata tuzo


Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Tanzania Distilleries imekabidhiwa tuzo ya viwango vya uzalishaji na usambazaji wa vinywaji vikali na mvinyo. Tuzo hiyo ilitolewa na Trade Leader's Club ambayo ina wanachama zaidi ya 7,000 duniani ambapo makao yake makuu yako mjini Madrid, Hispania. Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo hivi karibuni, Rais wa Trade Leader's Club, Arsenio Rodriguez alisema kampuni hiyo imeshindwa tuzo hiyo kutokana na uwezo wake katika uandaaji na usambazaji wa bidhaa zake. Jumla ya kampuni 24 duniani zilishiriki katika shindano hilo ambapo tuzo ya mwaka huu ambayo ni ya 27 ilitolewa kwa kampuni mbili toka Afrika nyingine ikiwa kutoka Mali. Meneja ufundi wa kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleres Ltd, Khadija Madawili akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam juzi alisema tuzo iliyonyakuliwa na kampuni hiyo ni changamoto ya kuhakikisha ubora wa bidhaa zake unakuwa endelevu. Alisema uongozi bora wa kampuni, motisha kwa wafanyakazi, kuwajali wateja na kujua upungufu na uwezo wa kampuni ni mambo yaliyozingatiwa na kusaidia kufikia ufanisi ndani ya kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...