Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 12, 2011

MWENYEKITI TUGHE NHIF ATEULIWA MJUMBE WA BARAZA LA WADHAMNI TUGHE TAIFA


Mpiganaji Baraka Maduhu mwenye koti jeusi ambaye ni mjumbe wa kuteuliwa kwenye baraza la wadhamini la TUGHE Taifa (National Tughe Board of Trustees) kutoka tawi la NHIFwakishikana mikono kuashiria mshikamano daima (SOLIDARITY FOREVER) katika kusimamia haki wajibu na sheria za kazi kwa watumishi wa Sekta ya Afya na Serikali Kuu,wakati wakitambulishwa kwenye ofisi za Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani kulia mwenye kofia ni katibu wa chama hicho Bwn.Kiwenge A.Kiwenge na Mwenyekiti Dkt. Mrutu.uteuzi huo ulifanywa hivi karibuni na kuhusisha matawi yaliyopo kwenye mikoa sita nchi nzima na kwa Dar es salaam inawakilishwa na bwn. Maduhu.
Wakipanga mikakati jinsi ya kusimamia majukumu waliokasimiwa kwenye Baraza la Wadhamini la TUGHE Taifa hili kuhakikisha maslahi ya watumishi wa Sekta ya Afya na Serikali Kuu yanakwenda sanjari na mabadiliko ya kiuchumi katikati ni mwenyekiti wa tawi la tughe NHIF Bwn. Baraka Maduhu ambaye Ameteuliwa rasmi hivi majuzi kuwa mmoja wa wadhamini wa baraza hilo kitaifa.hongera mpiganaji kwa kupewa nafasi hiyo na uwakilishi mwema.
Katika picha ya pamoja nje ya Makao Makuu ya ofisi ya Tughe Taifa zilizopo Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kushoto ni Bwn J. Mwankenja ambaye ni mteuliwa mwenza kitaifa anayemfuatia ni kamanda Baraka Maduhu Mwenyekiti TUGHE NHIF,kushoto kwake katibu wa Tughe Mkoa wa Pwani mzee kuyunga na mwisho kabisa ni bi Fortunat Raymond mwenyekiti kamati ya wanawake TUGHE NHIF.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...