Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 7, 2011

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO WAONJA JOTO LA NHC

IKIWA ni katika muendelezo wa kukusanya madeni na kuwatoa wadeni wake Shirika la Nyumba (NHC)leo asubuhi rungu lao lilitua katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) ambapo wafanyakazi wake wamejikuta wakilazimika kutoka nje kutokana na kudaiwa kodi ya miezi saba ambayo ni kiasi cha sh.mil.47 Ilifahamika kuwa Kodi ya mwezi waliyotakiwa kulipa ni sh.mil7,149,000.Kabla ya MAELEZO kupatwa na kadhia hiyo NHC walianza katika ofisi ya Utamaduni ambako wanadaiwa sh mil87
Mwandishi kutoka Kituo cha Star TV akalazimika kufanya mahojiano na kikundi kilichokwama kufanya mkutano ndani ua Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO.
Baazi ya wapagazi wakiwa wamesimama kidogo katika zoezi linaloendelea la kutoa vitendea kazi vya MAELEZO Dar es Salaam leo zoezi ambalo linaendeshwa na NHC la kuwatoa kwa nguvu wadeni wao.
Ofisa wa Shirika la Nyumba akiomwonyesha mwandishi wa habari kutoka gazeti la Majira Mohammed Mambo karatasi iliyokuwa ikionyesha kiasi cha kodi wanachodaiwa MAELEZO na NHC.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...