Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, October 31, 2011

Blogu Ya 8020 Fashion Yatimiza Miaka 5 Ya Utendaji Wake
Shamimu Mwasha mmiliki wa 8020 Fashion akimlisha keki mgeni rami Mh Angela Kairuki wakati wa hafla ya blogu hiyo kutimiza miaka 5 ya utendaji wake wa kazi.
Mmiliki wa Blogu ya mavazi ya 8020 Fashions Shamimu Mwasha kushoto aka Shamimu Zeze pamoja na mgeni rasmi Mbunge wa CCM viti maalum Dar es salaam Agela Kairuki wakizundua nembo ya mavazi ya B2A itakayomilikiwa na Shamimu, wakati wa hafla ya kutimiza miaka 5 ya mtandao wa 8020 Fashions iliyofanyika kwenye ukumbi wa Daimond Jubilee jijini Dar es salaam leo mchana.
Tukio hilo limedhaminiwa na kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa kusaidia wanawake MMWEI na kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers kupitia kinywaji chake kikali cha Baileys
hamimu Mwasha mmiliki wa 8020 Fashion na mgeni rasmi Mh Angela Kairuki wakiangalia mavazi ya nguo zilizobuniwa kwa kutumia nembo ya mavazi ya B2A kama wanavyoonekana
Wageni waalikwa katika hafla hiyo wakijimwaga stejini kucheza muziki kama wanavyoonekana katika picha.
Joseline Kamuhanda kushoto na Grace Lyon kutoka Vodacom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla hiyo.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania , Mwamvita Makamba kulia akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa MMWEI Vodacom Tanzania Mwamvua Mlangwa katika hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...