Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, October 10, 2011

Taswa FC yaharibu haribu sherehe za uzinduzi wa uwanja ya uwanja wa michezo wa Boko Beach


Mwandishi wetu
TIMU ya soka ya waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa FC leo iliharibu sherehe za uzinduzi wa uwanja ya uwanja wa michezo wa Boko Beach baada ya kuichabanga timu hiyo kwa mabao 4-1.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja huo, Said Seif alifunga mabao mawili akitumia pasi safi za Majuto Omary kutoka wingi ya kulia.
Mabao hayo yaliichanganya timu ya Boko beach veterans pamoja na kumchezesha Hussein Swed wa timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Kagera Sugar.
Taswa FC ilitawala sana mchezo huo na hadi mapumziko, timu hiyo ilikuwa mbele kwa mabao 2-0. Kipindi cha pili, Boko ilifanya mabadiliko kwa asilimia 95 ya wachezaji wake na kuanza kipindi hicho kwa kasi.
Timu hiyo ilipata bao lake kupitia kwa Elly Alexander kufuatia kazi nzuri ya Swed. Bao hilo lilizua utata kutokana na waamuzi kupingana, mwamuzi wa pembeni akisema ni kona na wa kati kusema mpira huo umeingia wavuni.
Baada ya mabao hayo, Taswa FC ilikuja juu na kufunga bao la tatu kupitia kwa Hussein Omari kufuatia kazi nzuri ya Seif na bao la nne likifungwa na Ali Mkongwe kwa njia ya penati baada ya beki wa Boko Beach Veterans, Singbert Ndululu kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Katika michezo mingine, Rose Garden ililala kwa mabao 2-1 na Kunduchi na Sitakishari ilifungwa kwa mikwaju ya penati 4-2 dhidi ta TBL.
http://fullshangwe.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...