Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 7, 2011

Nishioka atetea taji lake WBC


Nishioka atetea taji lake WBC

LAS VEGAS,Marekani

MJAPAN Japan, Toshiaki Nishioka,amefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Shirikisho la Masumbwi Duniani (WBC),katika uzani wa super bantam, baada ya kumshinda mpinzani wake kwa pointi, Rafael Marquez, katika pambano lililofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye ukumbi wa MGM Grand,uliopo jijini Las Vegas nchini Marekani.

Shirika la Habaria la Marekani AP,lilieleza kuwa kwa ushindi huo, Nishioka ambaye atakuwa amefikisha ushindi mara 39-4-3 yakiwemo mapambano sita aliyokuwa akitetea ubingwa wake alipata pointi 117-111, 116-112 na 115-113 kutoka kwa majaji watatu na wakati Marquez atakuwa ameporomoka kwa ushindi wa 40-7.
“Mafanikio yangu ni kutokana na kutojiweka mbali na Marquez,”alisema bondia huyo mwenye umri wa miaka 35 kupitia kwa mkalimani.

. “Ana ngumi nzito za mbali.Marquez ni mzuri kwa kukwepa makonde na ni vigumu kukwepa makonde yake yenye nguvu.Hakuna dakika ambayo niliweza kupumzika,"aliongeza bondia huyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...