Meneja wa
Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionyesha baadhi ya vifaa
vitavyokabidhiwa kwa wajasiliamali waliofuzu katika grogramu ya ruzuku ya
“Wezeshwa na Safari Lager” Dar es Salaam jana.Vifaa hivyo vitakabidhiwa
mwishoni mwa wiki katika viwanja vya CCM
Ilomba Mkoani Mbeya.
Meneja wa
Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL)
kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi tarehe na zawadi
zitakazokabidhiwa kwa wajasiliamali ambazo ni vitendea kazi kwa wajasiriamali
walioshinda katika shindano la “Wezeshwa
na Safari Lager”.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo
alisema wajasiriamali watakabidhiwa ruzuku zao kwenye kanda walizofanyia
mafunzo ya ujasiriamali. Bwana Oscar alisema, “Tutaandaa matamasha ya
kuwazawadia wajasiriamali wetu ambapo tunawaalika pia wafanyabiashara wengine
wa eneo lao ili kufurahi pamoja na wajasiriamali wetu”. Aliendelea, “Kituo cha
Mbeya tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 02 June katika kiwanja cha
CCM Ilomba, kituo cha Arusha tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 09
June katika viwanja vya Soweto, kituo cha Mwanza tamasha litafanyika siku ya
Jumamosi tarehe 16 June katika kiwanja cha Furahisha na tutamaliza na kituo cha
Dar Es Salaam ambapo tamasha litafanyika siku ya Jumapili tarehe 23 June kwenye
viwanja vya leaders Club.”
Akielezea mchakato wa kuwapata
wajasiriamali hawa Bwana Shelukindo alisema baada ya kutangaza kuanza kwa
shindano hili mwishoni mwa mwaka jana, jumla ya fomu za maombi 9,738
zilikusanywa. Fomu hizi zilikaguliwa na majaji wenye ujuzi wa mambo ya biashara
na wajasiriamali 80 walichaguliwa kuingia katika hatua ya pili. Wajasiriamali
waliochaguliwa walitembelewa na wataalamu ili kuthibitisha uwepo wa biashara
zao, jumla ya wajasiriamali 54 walifaulu na ndio waliopatiwa mafunzo.
Wajasiriamali 26 waliondolewa katika hatua hii kutokana na mapungufu mbalimbali
kama kuomba kuwezeshwa wakati biashara sio za kwao, kutokuwa na biashara
inayoendelea .
Akionyesha baadhi ya ruzuku
zitakazotolewa kwa wajasirimali walioshinda bwana Oscar alisema, “wajasiriamali
wetu wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wako
wajasiriamali katika fani tofauti pia kama Mafundi wa kushona nguo za aina
tofauti, mafundi seremala, magari nk
wako pia wajasiriamali wa kusindika vyakula, ufugaji wa samaki, ufugaji wa
kuku, kutengeneza mizinga ya nyuki nk, wako wajasiriamali katika biashara za
vyakula, kuuza vinywaji, umeme jua, teknolojia ya mawasiliano .
Bwana Shelukindo aliwataja tena wajasiriamali
watakaopatiwa ruzuku ya vitendea kazi ili kupanua biashara zao. Katika kituo cha
Dar Es Salaam wajasiriamali watakaokabidhiwa ruzuku ni Catherine Urio,
Josephine Kisiri, Zainabu Juma Zayumba, Elizabeth Chami, Richard Kwiligwa,
Hilary Meck Mremi, Damas Daniel Msoka, Innocent Mbelwa, Stumai Namanga, Dasina
J Buzuka, Christabela Lymo, Dadan J Munisi, Faraji Bakary Mgwegwe, Issa Lema na
Valerian Tigano Luzangi. Shelukindo aliwataja pia washindi wa kituo cha Arusha
kuwa ni Ansilla Danny, Bibie Msumi, Rogers Msangi, Simon Kinabo, Sophia
Khalfan, Yuda Mbando, Amani Lymo, Adam Akilinyingi, Joseph M. Mnemwa, Rose
Tesha na Victoria Riwa.
Bwana Shelukindo aliendelea kuwataja
wajasiriamali watakaojipatia ruzuku katika kituo cha Mwanza ambao ni Bora
Mganda, Brighton Dismas Maricell, Mangana Kilahanya Kigombe, Prudence Mubito,
Musa Mahushi George, Innocent K. Doi, Amos Edward Mwambola, Edith Mudogo, Aron
Magembe, Yusuph A. Kawaga, Zamda Shabban, Oscar Bosco Kabobo, Yahaya Fundisa,
Dainess Ngaiza na Boniface Joseph Minja. Na katika kituo cha Mbeya
wajasiriamali waliofaulu kupata ruzuku baada ya mafunzo ni Rose Eliudi Maruila,
Benedict Abel Matandiko, Vumilia Mtweze, Bahati Mbata, Hellen A. Mwanguku,
Felix Phillip Kamuhabwa, Festo Mwakasege, Phares Richard Lymo, Iradi A. Msemwa,
Gabriel Mwalugaja na Tatu Ngemela. Jumla ya ruzuku ya vitendea kazi vya thamani
ya shilingi milioni 200 vitatolewa kwa wajasiriamali hawa.
Bwana Shelukindo alimaliza kwa
kuwashukuru watanzania wote kwa kushiriki shindano la Wezeshwa na Safari Lager,
alisema “Shukrani nyingi ziende pia kwa wanywaji wetu wa bia ya Safari Lager,
bila wao hakika zoezi zima la Wezeshwa na Safari Lager lisingewezekana,
tunawaomba waendelee kufurahia bia yetu”. Aliwakaribisha kuhudhuria matamasha
haya na aliwaomba radhi wajasiriamali ambao hawakufaulu, na wale wanaoendelea
kutuma fomu wasitume tena, wajiandae kushiriki shindano lijalo la Wezeshwa na
Safari Lagerbaadae mwaka huu
Meneja akizungumza na waandishi wa habari