Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 29, 2012

MSANII WA BONGO FLAVA KASSIM MGANGA AWAPAGAWISHA MASHABIKI WA EXTRA BONGO MEEDA


 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Kassim Mganga, (kushoto) akiimba katika jukwaa moja na wanamuziki wa bendi ya Extra Bongo wakati wa onyesho la bendi hiyo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Meeda uliopo Sinza Dar es Salaam. Mashabiki wa bendi hiyo walisikika kumshangilia baada ya kupanda jukwaani na kuimba kipande cha wimbo wa Rejina Zanzibar, huku wengine wakimtaka kuendelea kuimba bila kushuka jukwaani hapo.

 'Mkaanga Chips' Martine Kibosho, akizicharaza Drams, kwa umahiri mkubwa wakati wa onyesho lao hilo.
 Mwimbaji wa Bendi hiyo, Bob Kissa, akiimba jukwaani.
 Huyu yeye ni kiraka katika bendi hiyo, kwani anauwezo wa kuimba, kurap, kupiga Tumba na kucheza, ambapo ndani ya bendi hii ni Kiongozi wa Wanenguaji na tayari ametunga wimbo wake utakaokuwa ndani ya albam ya bendi hiyo ijayo unaokwenda kwa jina la Bakutuka.
 Mpiga Gitaa la Besi, mahiri Hosea Bass, akiliungirumisha gitaa katika onyesho hilo.
Wanenguaji wa bendi hiyo wakishambuliwa jukwaa wakati wa onyesho lao na kuwapagawisha mashabiki wao ambao kamwe hawakuvumilia kuketi vitini bali waliamka kila dakika na kwenda kuwatunza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...