Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 30, 2012

AMOSI MAKALA AKABIDHI BENDERA KWA WACHEZAJI WA GOFU


Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala ameitaka timu ya Taifa ya Wanawake ya gofu kuhakikisha inapeperusha vyema bendera ya nchi katika mashindano ya All Africa Challenge yanayotarajia kuanza Juni 5, Botswana.

Timu hiyo inatarajia kuondoka nchini kesho kutwa huku ikiwa na Wachezaji watatu sambamba na mkuu wa msafara ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Maendeleo na watoto ya bunge Mary Chitanda.

Timu hiyo inaondoka nchini ikiwa tayari imeisha wahi kushika nafasi ya pili katika mashindano hayo yaliyofanyika mwaka 2010 ambapo hufanyika kila baada ya miaka miwili.

Akizungumza Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo Makala alisema watumie matoke hayo ya awali kwa kufanya vyema zaidi na kuweza kupeperusha vyema bendera ya nchi.

"Kama katika taarifa yenu ionavyosema mashindano ya mwisho mlishika nafasi ya pili sasa tunaimani mashindano haya mtakuwa wa kwanza na kuweza kututangaza vyema katika bara hili la Afrika, hivyo nendeni makaipiganie nchi yenu na kwa manufaa ya michezo," alisema.

Naye kwa upande wake Kepteni wa timu hiyo Madina Idd alisema kama waliweza kushika nafasi hiyo ya pili na wakati huo walikuwa katika maandalizi mabovu hivyo kwa sasa wanawahakikishia Watanzania wataibuka na ushindi.

"Mwaka 2010 tulishiriki na hata kufanikiwa kushika nafasi hiyo na huku tulikua katika maandalizi ya kusuasua lakini kwa sasa naimani tutafanya vyema zaidi," alisema.

Sambamba na hilo Shirika la ndege la Precion Air leo limekabidhi tiketi saba kwa timu  hiyo zikiwa ni za kwenda na kurudi ikiwa ni pamoja na tisheti na kofia vyote vikiwa na jumla ya sh. milion 7.3.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...