Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 25, 2012

TIMU YA ASHANTI YA ILALA NA POLISI MARA KUFUNGUA PAZIA LA LIGI KUU


Michuano ya Ligi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa inaanza Mei 27 mwaka huu katika vituo vitatu tofauti huku Ashanti United ya Ilala na Polisi ya Mara zikifungua dimba katika Kituo cha Musoma.
 
Ligi hiyo ambayo inatarajia kumalizika Juni 12 na 13 mwaka huu itashuhudia mechi mbili kwa siku katika kila kituo, huku ya kwanza ikichezwa saa 8 mchana na kufuatiwa nay a pili 10 jioni.
 
Mechi za ufunguzi Kituo cha Musoma ambapo mechi zake zitachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma ni Flamingo ya Arusha dhidi ya Forest ya Kilimanjaro (saa 8 mchana) wakati saa 10 jioni ni Ashanti United na Polisi.
 
Kituo cha Kigoma siku ya ufunguzi kutakuwa na mechi moja tu itakayoanza saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika kati ya Mwadui ya Shinyanga na JKT Kanembwa ya Kigoma. Siku inayofuata ni CDA (Dodoma) vs Majimaji ya Tabora (saa 8 mchana) na Bandari ya Kagera vs Pamba ya Mwanza (saa 10 kamili jioni).
 
Tenende ya Mbeya na Kurugenzi ya Iringa ndizo zitakazoanza saa 8 mchana kwenye Kituo cha Mtwara na kufuatia na mechi kati ya Mpanda Stars ya Rukwa na Ndani ya Mtwara kuanzia saa 10 kamili jioni. Mechi hizo zitachezwa katika Uwanja wa Umoja.

1 comment:

  1. EEEBWANA HIVI SASA HALI NI MBAYA JUU YA POLISI DHIDI YA RAIA HALI INATISHA NI UNYANYASAJI MTUPU INANIUMA SANA ILA NASHINDWA NA KUNA HAWA POLISI JAMII NA WAGAMBO KAZI YAO KUTESA NA KUCHUKUA RUSHWA KWA RAIA TOA KOMENTI YAKO

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...