Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 22, 2012

MSONDO KUTOA BURUDANI KATIKA UKUMBI WA EMIRATE MASDASI JUNE 2
Na Mwandishi Wetu

BENDI Kongwe ya Msondo ngoma ya jijini Dar es salaam inatalajia kufanya uzinduzi wa ukumbi mpya kabisa wa kisasa wa burudani  wa Emirate Hall uliopo Masasi June 2 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' Alisema wamealikwa kwa ajili ya kutoa burudani siku ya ufunguzi wa ukumbi huo ambapo watatoa burudani isiyo na kifani

;unajua sisi ni baba ya Muziki nchini ndio mana wapenzi wengi wanaitaji burudani kutoka kwetu ndio mana tunapopata nafasi ya kwenda mikoani tunakwenda kama hivi tumealikwa kutoa burudani siku hiyo tutatoa burudani

ya uwakika;

siku hiyo tutapiga vibao vetu vya zamani na vipya kwa sasa alivitaja baadhi ya vibao vitakavyonogesha uzinduzi huo kuwa ni Suluhu wa Shabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa Eddo Sanga hizo ni baadhi ya nyimbo mpya zitakazonogesha siku hiyo vile vile watapiga nyimbo zao za zamani
zilizotamba wakati huo  Alisema Super D Kundi hilo litaambatana na wanamziki wake wote wakiwemo wakongwe katika mziki wa Dansi Nchini Maalimu Gulumo ' Kamana' Saidi Mabela ' DKT Mabela' na wengine wote watafanya vitu vyao siku hiyo kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wao wa Masasi Aliongeza Super D

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...