Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 30, 2012

THABEET KUFUNDISHA KIKAPU WATOTO 200NYOTA wa NBA, Hasheem Thabeet anategemea kutoa mafunzo ya siku mbili ya kucheza mpira wa kikapu kwa watoto 200 walio chini ya miaka umri wa miaka 17 kwenye  Uwanja wa Don Bosco kuanzia Juni 2 hadi Juni 3.

Thabeet anayechezea timu ya Portland Trail Blazers inayoshiriki Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) ataongoza kliniki hiyo yenye lengo la kuibua vipaji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,Thabeet alisema  mafunzo ya mwaka huu yatakuwa ni tofauti kidogo na yale ya mwaka jana.

“Ninaimani kliniki hii itakuwa tofauti na ile iliyopita kwa sababu watoto wengi wamepata mwamko wa kucheza mpira wa kikapu baada ya kuona mafanikio ya wenzao,”anasema Thabeet.

Naye Meneja wa Sprite nchini Warda Kimaro wanadhamini wa mashindano hayo alisema baada ya mafunzo hayo vijana hao watakuwa kwenye mpango maalum wa kuendelezwa na kampuni yake.


Habari - Jackson Odoyo
Picha - globalpublishers.info

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...