Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 23, 2012

MISS CHANG'OMBE KURINDIMA JUNI 9 MWAKA HUU UKUMBI WA QUALITY CENTREMashindano ya kuwania taji la Redds Miss Tanzania 2012 yanazidi kupamba moto kwa ngazi za vitongoji nchini kote huku vitongoji kadhaa vikiwa tayari vimeshafanya mashindano yake na vingine vikiendelea na maandalizi.

Wakati wiki hii Mashindano hayo yakitraji kufanyika katika Vitongoji vya Kurasini Jijini Dar es Salaam tayari Warembo wanaowania taji la Redds Miss Cha'gombe 2012 nao wapo katika mazoezi kujiandaa na fainali zao zitakazofanyika Juni 9 mwaka huu katika Ukumbi wa Quality Centre, jijini Dar es Salaam.

Pichani ni warembo wa Chan'gombe wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi yao jana jioni katika ukumbi wa TCC Chang'ombe .

Warembo hao 11 wanataraji kupanda jukwaani mapema mwezi ujao kuwania taji hilo na kuwania tiketi ya kushiriki Miss Temeke 2012. Picha na Father Kidevu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...