Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 23, 2012

Waziri Amos Makala akutana na wananchi kujadili mgogoro wa Ardhi Kinyenze


Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( aliyesimama na kunyosha mkono juu) akisisitiza jambo juu ya namna ya kutafuta muakafa ili kumalizwa kwa mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kitongoji cha Kinyenzi dhidi ya Mwekezaji wa kizungu.
(Picha kwa Hisani ya FATHER KIDEVU BLOG)
Mzee Said Ahamad Kondo ( aliyesimama) akiuliza maswali kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Mvomero , Amos Makalla ( hayupo pichani) alipokuwa katika Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali kufuatilia mgogoro kati ya Wananchi hao na Mwekezaji wa Kizungu.
Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Mvomero, Majaliwa Jafari ( aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa mgogoro wa shamba namba shamba 296 kati ya wanachi wa Kitongoji cha Kinyenze na Mwekezaji wa Kizungu kwenye mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo , uliofanyika hivi karibini ( Mei 19) uliokuwa na lengo la kufikia utatuzi wa mgogoro huo
Baadhi ya wazee na wananchi wa Kitogoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera,Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo hilo, Amos Makalla ( hayupo pichani) wakati akipowatembelea hivi karibuni ( Mei 19) wananchi wa Kitongoji hicho kwa ajili ya kupanga mkakati wa kumalizwa mgogoro kati ya mwekezaji wa kizungu na wakazi hao, Mbunge huyo pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...