Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 23, 2012

Taarifa kwa Vyombo vya Habari 23 Mei, 2012, Dar es Salaam. Tigo imetangaza uzinduzi wa promosheni inayoipa pesa yako thamani, ijulikanao kama ‘Xtreme Pack’, kwa ajili ya mawasiliano ya jumla, yanayopatikana muda wowote na wakati wowote.
 Kwa kupiga *148*01# au kutuma neno XTREME kwenda namba 15509, wateja wa huduma ya kulipia kabla watafurahia huduma za thamani ambazo ni pamoja na dakika 15 za muda wa maongezi zitakazowawezesha kupiga simu Tigo kwa Tigo, sms 100, 50 MB kwa ajili ya kuperuzi facebook, kutumia mtandao, E-mail pamoja na Twitter, vyote hivyo kwa gharama ya Tsh 450 na kuokoa Tsh 4,600!  Pia tigo itatuma ujumbe mfupi wa maneno bure kwa wateja wao, kuwataarifu juu ya ukomo wa matumizi ya vifurushi vyao na kuwaruhusu kujiunga tena kama watahitaji .
“Tunatafuta njia thabiti ya kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma zinazoendana na thamani ya pesa zao” alisema Alice Maro ambaye ni afisa uhusiano wa Tigo. “Kwa kupitia promosheni hii mpya wateja wataweza kutumia huduma za kusisimua kutoka simu za apps, ambazo huduma na maudhui yake huboresha maisha, kazi na starehe zao. Kuridhika kwa mteja ni kitu cha muhimu sana katika biashara yetu, na ndio maana tunahakikisha kuwa tunabuni huduma na bidhaa zinazoridhisha na kuendana na matakwa ya mteja,” alisema.
Tigo imeanzisha promosheni za kuaminika na zenye uwazi kwa kufanya mawasiliano kuwa sio rahisi tuu kutumia bali zenye thamani.
Kuhusu Tigo:
Tigo ni mtandao wa simu za mkononi wa kwanza Tanzania, ulianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini unaotoa huduma katika mikoa 26, Tanzania Bara na Zanzibar. 
Tigo ni sehemu ya Millicom International Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 43 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.
Kwa taarifa zaidi tembeleawww.tigo.co.tz


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...