Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 23, 2012

RADO ATOKA NA FILAMU MPYA YA TAMAA YANGU

Na Mwandishi Wetu


MSANII wa filamu nchini Simoni Mwapagatwa 'Rado' ameibuka na filamu Mpya inayokwenda kwa jina la Tamaa yangu Nguvu za giza filamu hiyo inayotarajia kuingia sokoni  wakati wowote kuanzia sasa filamu hiyo yenye ujumbe maususi kwa jamii inayozungumzia tamaa ambapo mtu ujiingiza katika mambo ambayo yasiyo staili kwa jamii na kujikuta anajingiza katika mambo makubwa zaidi ya kishirikina

Rado ambaye anaonekana kuishi katika maisha ya kifukala na kukutana na rafiki yake kipenzi Single Mtambalike 'Rich Rich' ambaye anamshawishi kwenda kwa mganga na anambiwa masharti ya mganga ni lazima utembee na mama yako mzazi Rado ana kataa anaporudi kwa RIchi anamwambia sina uwezo wa kukusaidia

Ndipo anapofanya maamuzi ya kulala na mama yake mzazi na kufanikiwa kuwa tajiri ambapo mama yake anapotambua kuwa amelala na mwanae anamua kujiuwa ili kuondokana na aibu hiyo

Filamu hiyo itakayokuwa ikisambazwa na Kampuni ya SPLASH ya jijini Dar es salaam itakua mtaani wakati wowote kuanzia leo katika filamu hiyo iliyowashirikisha wakari wengine kama Regina Mroni, Deogratus Shija na wengine wengi waliyonogesha filamu hiyo ambayo si ya kukusa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...