Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 29, 2012

BAADA YA KUTANGAZWA KUTIMULIWA TWANGA PEPETA MARTINE SOSPETER ATANGAZA KUJIUNGA NA BENDI YA MASHUJAA


Aliyekuwa Meneja wa Bendi ya Twanga Pepeta, Martin Sospeter (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Busness uliopo Kijitonyama wakati akitoa malalamiko yake kuhusu tuhuma zilizoelezwa ndiyo chanzo cha kufukuzwa katika bendi ya Twanga majuzi, (kulia)  ni Kaimu Meneja wa bendi ya Mashujaa Muzika King Dodoo (kushoto) ni Rais wa Bendi ya Mashujaa Charles Baba.
****************************************
Akizungumza na waandishi wa habari Martine, alisema kuwa ''Juzi usiku nilishangazwa na kauli ya mkurugenzi wangu wa zamani, Asha Baraka, katika taarifa aliyoitoa katika vyombo vya habari  na mitandao ya kijamii kuwa amenifukuza kazi kutokana kuihujumu bendi ikiwemo kushawishi wanamuziki kujiunga na bendi ya Mashujaa,

Kwa kweli kauli ile ilinisikitisha sana kutokana na ukweli kwamba Asha, nilimchukulia kama zaidi ya dada kwani nilifanya naye kazi kwa  miaka 14 iweje hii leo aje anitolee maneno ya kunichafua katika vyombo vya habari?,

Mimi sijawahi kuhusika na mpango wowote wa wasanii wa Twanga kuhamia Mashujaa na wala sikuwa nafahamu mpango huo zaidi ya mwisho wa siku kusikia fununu za chinichini na mwishowe wasanii hao kutanghazwa kuhamia Mashujaa.

Leo napenda nitangaze rasmi kwamba nimeachana na African Stars na kujunga na Mashujaa Entertainment na tayari nimeshasaini mkataba wa kazi katika bendi hii, 

“Nilipanga nifanye taratibu za kumuaga kutokana na kuwa nilikuwa nafanya kazi kwake bila ya mkataba lakini nimepata bendi hii ambayo tulikaa na kukubaliana mambo kadhaa na kuona kuwa yana maslahi kwangu, 

Mbali na mkataba baadhi ya makubaliano na uongozi wa mashujaa ni pamoja na kunipangishia nyumba hali itakayonilazimu kuhama ile iliyokuwa chini ya Twanga.

Ninaamini nitafanya vizuri kazi zangu katika bendi hii mpya kama ilivyokuwa Twanga ambapo nilidumu kwa muda mrefu na kuchangia kufika hadi hapo nilipoachia, hivyo naomba ushirikiano kwa uongozi, wanamuziki, Wadau na hata ninyi wanahabari.

KUNANI WANAMUZIKI WOTE KUTIMKA TWANGA NA KUJIUNGA NA MASHUJAA??

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...