Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 23, 2012

MAHAKAMA YAMGOMEA KAJALA HAKIMU MPYA


Kajala Masanja kuli, akiwa amejifunika usoni na kushoto katika pozi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya msanii wa filamu nchini Kajala Masanja na mumewe Faraja Chambo ya kutaka kesi yao ihamishiwe kwa hakimu mwingine ili iweze kuendelea kusikilizwa. 
Kajala na mumewe waliwasilisha maombi hayo baada ya kupokea taarifa kuwa hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi yao Sundi Fimbo yupo likizo ya uzazi . 
Maombi yao yalitupiliwa mbali na Hakimu Frank Moshi ambaye alisema amepokea jalada la kesi hiyo kwa ajili ya kutoa ufafanuzi. 
“Nimewasiliana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama Ilvin Mgeta , amesema kwa kawaida shauri halifanyiwi mabadiliko iwapo hakimu yupo likizo na kwamba huo utakuwa ni usumbufu,” alisema hakimu huyo. 
Baada ya uamuzi huo alipanga kesi hiyo iahirishwe hadi Juni 5, mwaka huu itakapotajwa mpaka hakimu atakapomaliza likizo yake. 
Kajala Masanja na mumewe Faraja Chambo wanakabiliwa na mashtaka matatu kula njama, kuhamisha umiliki wa nyumba na kutakatisha fedha haramu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...