Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, May 31, 2012

SAFARI LAGER YATANGAZA TAREHE NA ZAWADI ZITAZOKABIDHIWA KWA WAJASILIAMALI WASHINDI WA “WEZESHWA NA SAFARI LAGER”.


  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionyesha baadhi ya vifaa vitavyokabidhiwa kwa wajasiliamali waliofuzu katika grogramu ya ruzuku ya “Wezeshwa na Safari Lager” Dar es Salaam jana.Vifaa hivyo vitakabidhiwa mwishoni mwa wiki katika viwanja  vya CCM Ilomba Mkoani Mbeya.
  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi tarehe na zawadi zitakazokabidhiwa  kwa wajasiliamali  ambazo ni vitendea kazi kwa wajasiriamali walioshinda katika shindano la “Wezeshwa na Safari Lager”.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema wajasiriamali watakabidhiwa ruzuku zao kwenye kanda walizofanyia mafunzo ya ujasiriamali. Bwana Oscar alisema, “Tutaandaa matamasha ya kuwazawadia wajasiriamali wetu ambapo tunawaalika pia wafanyabiashara wengine wa eneo lao ili kufurahi pamoja na wajasiriamali wetu”. Aliendelea, “Kituo cha Mbeya tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 02 June katika kiwanja cha CCM Ilomba, kituo cha Arusha tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 09 June katika viwanja vya Soweto, kituo cha Mwanza tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 16 June katika kiwanja cha Furahisha na tutamaliza na kituo cha Dar Es Salaam ambapo tamasha litafanyika siku ya Jumapili tarehe 23 June kwenye viwanja vya leaders Club.”
Akielezea mchakato wa kuwapata wajasiriamali hawa Bwana Shelukindo alisema baada ya kutangaza kuanza kwa shindano hili mwishoni mwa mwaka jana, jumla ya fomu za maombi 9,738 zilikusanywa. Fomu hizi zilikaguliwa na majaji wenye ujuzi wa mambo ya biashara na wajasiriamali 80 walichaguliwa kuingia katika hatua ya pili. Wajasiriamali waliochaguliwa walitembelewa na wataalamu ili kuthibitisha uwepo wa biashara zao, jumla ya wajasiriamali 54 walifaulu na ndio waliopatiwa mafunzo. Wajasiriamali 26 waliondolewa katika hatua hii kutokana na mapungufu mbalimbali kama kuomba kuwezeshwa wakati biashara sio za kwao, kutokuwa na biashara inayoendelea .
Akionyesha baadhi ya ruzuku zitakazotolewa kwa wajasirimali walioshinda bwana Oscar alisema, “wajasiriamali wetu wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wako wajasiriamali katika fani tofauti pia kama Mafundi wa kushona nguo za aina tofauti,  mafundi seremala, magari nk wako pia wajasiriamali wa kusindika vyakula, ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, kutengeneza mizinga ya nyuki nk, wako wajasiriamali katika biashara za vyakula, kuuza vinywaji, umeme jua, teknolojia ya mawasiliano .
Bwana Shelukindo aliwataja tena wajasiriamali watakaopatiwa ruzuku ya vitendea kazi ili kupanua biashara zao. Katika kituo cha Dar Es Salaam wajasiriamali watakaokabidhiwa ruzuku ni Catherine Urio, Josephine Kisiri, Zainabu Juma Zayumba, Elizabeth Chami, Richard Kwiligwa, Hilary Meck Mremi, Damas Daniel Msoka, Innocent Mbelwa, Stumai Namanga, Dasina J Buzuka, Christabela Lymo, Dadan J Munisi, Faraji Bakary Mgwegwe, Issa Lema na Valerian Tigano Luzangi. Shelukindo aliwataja pia washindi wa kituo cha Arusha kuwa ni Ansilla Danny, Bibie Msumi, Rogers Msangi, Simon Kinabo, Sophia Khalfan, Yuda Mbando, Amani Lymo, Adam Akilinyingi, Joseph M. Mnemwa, Rose Tesha na Victoria Riwa.
Bwana Shelukindo aliendelea kuwataja wajasiriamali watakaojipatia ruzuku katika kituo cha Mwanza ambao ni Bora Mganda, Brighton Dismas Maricell, Mangana Kilahanya Kigombe, Prudence Mubito, Musa Mahushi George, Innocent K. Doi, Amos Edward Mwambola, Edith Mudogo, Aron Magembe, Yusuph A. Kawaga, Zamda Shabban, Oscar Bosco Kabobo, Yahaya Fundisa, Dainess Ngaiza na Boniface Joseph Minja. Na katika kituo cha Mbeya wajasiriamali waliofaulu kupata ruzuku baada ya mafunzo ni Rose Eliudi Maruila, Benedict Abel Matandiko, Vumilia Mtweze, Bahati Mbata, Hellen A. Mwanguku, Felix Phillip Kamuhabwa, Festo Mwakasege, Phares Richard Lymo, Iradi A. Msemwa, Gabriel Mwalugaja na Tatu Ngemela. Jumla ya ruzuku ya vitendea kazi vya thamani ya shilingi milioni 200 vitatolewa kwa wajasiriamali hawa.
Bwana Shelukindo alimaliza kwa kuwashukuru watanzania wote kwa kushiriki shindano la Wezeshwa na Safari Lager, alisema “Shukrani nyingi ziende pia kwa wanywaji wetu wa bia ya Safari Lager, bila wao hakika zoezi zima la Wezeshwa na Safari Lager lisingewezekana, tunawaomba waendelee kufurahia bia yetu”. Aliwakaribisha kuhudhuria matamasha haya na aliwaomba radhi wajasiriamali ambao hawakufaulu, na wale wanaoendelea kutuma fomu wasitume tena, wajiandae kushiriki shindano lijalo la Wezeshwa na Safari Lagerbaadae mwaka huu
 .
Meneja akizungumza na waandishi wa habari

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...