Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, May 28, 2012

BIA YA CASTLE LITE SASA IPO YA KOPO


Kopo jipya la Castle Lite linavyoonekana sasa
Bia maarufu ya Castle Lite, inayozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imezindua rasmi muonekano wa kopo lililojazwa kinywaji hicho ikiwa ni muendelezo wa kuwarahisishia walaji upatikanaji wa Bia hiyo iliyotokea kupendwa na watumiaji wa vileo na kuifanya iwe bia inayokua kwa kasi hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Castle Lite Bi. Pamela Kikuli alisema; Leo tunazindua ujazo mpya wa bia ya Castle lite, bia yenu muipendayo kwa sasa inapatikana katika kopo lenye ujazo wa mililita 330. Uamuzi huu unatokana na mahitaji makubwa toka kwa watumiaji na wapenzi wa bia hii ambayo imekuwa ikipatikana katika chupa yenye ujazo wa mililita 375.

 Wateja wetu walihitaji kuipata bia yao popote pale walipo au kuwa nayo popote waendapo, hivyo kupatikana kwa bia hii katika chupa peke yake kulipunguza uhuru wa kuwa na bia yao popote waendapo kwani walihitaji kurudisha chupa kila waitumiapo.

Uzinduzi wa Castle lite ya kopo utasaidia zaidi kuongeza upatikanaji wa kinywaji hiki katika maduka ya reja reja (super markets) n.k kote nchini na kuwapa nafasi wapenzi wa castle lite kununua bia yao waipendayo na kwenda nayo nyumbani. Bei ya reja reja kwa kopo ni shilingi 1700/- na bei ya reja reja kwa chupa itaendelea kubaki ile ile 1700/-.

Kwa upande wake Meneja mawasiliano na mahusiano ya jamii wa Tbl Edith Mushi aliwashukuru wapenzi na watumiaji wa bia ya Castle Lite kwa kuweza kuipa mafanikio makubwa katika soko la bia hapa nchini, “ninawahakikishia kuwa mnafanya uamuzi ulio sahihi kwa kuchagua kutumia Castle Lite” nasi tutaendelea kuwapatia bia iliyo bora siku zote. Alisema Edith.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...