Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, May 21, 2012

ROMA MKATOLIKI AFUNIKA MBEYA


 

 Roma Mkatoliki akitumbuiza jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award jijini Mbeya katika Uwanja wa Sokoine jana.Picha zote naFather Kidevu Blog
 Suma Lee nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuleta raha kwa mashabiki katika wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music jijini Mbeya
 Ben Paul nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuletya raha kwa mashabiki katika wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award jijini Mbeya.
 Barnaba Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimbo jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award jijini Mbeya katika Uwanja wa Sokoine
 Vijana wengi walikuwa wamepigilia vitu vya namna hii
 Mashabiki walikuwa hawatulii
Mkali wa Bongo fleva Ali Kiba  akiimba jukwaani hii wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika uwanja wa Sokoine 
 Wasichana waliokuwa wakitoa huduma ya tiketi
 Mkali wa Bongo fleva Ali Kiba akiimba na Omy Dimpoz katika wimbo Nai Nai akiimba jukwaani hii wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika uwanja wa Sokoine.Picha zote na Father Kidevu Blog
Dimpoz kwa Pozi akipitika katikati ya wacheza show wake.
 Msanii AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza sho wake wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award  jijini Mbeya katika Uwanja wa Sokoine jana
Na  Father Kidevu Blog, Mbeya.
MANENO ya Injili yanayosema wa mwisho anakuwa wa kwanza na wa kwanza anakuwa wa mwisho yametima jana katika Uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya pale mkali wa Hip Hop,  Roma  Mkatoliki alipoongoza jahazi la wakali wa Tuzo za Kili Musc Award 2012 katika onesho lao la Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya jana.
Roma akipanda juukwaani akisindikizwa na DJ maarufu DJ Choka, alishangiliwa vilivyo na umati wa watu uliofurika uwanjani hapo pale tu ilipofika zamu yake kupanda jukwaani.
Roma! Roma! Roma! Roma!....hayo ndio yalikuwa maneno ya shwangwe kutoka kwa wapenzi wa burudani kutoka Jijini Mbeya waliofurika katika Uwanja wa Sokonine mjini hapa kushuhudia show hiyo kali ya Washindi wa Tuzo za Kili Music Award 2012.
Roma baada ya kumaliza kuimba nyimbo zake kaza aliwashukuru wana Mbeya kwa kura zao zilizompa ushindi na kuwaambia sasa anamaliza show hiyo ambayo hadi hapo alipofikia alisema wametumia Sh 200/= pekee kati ya Sh 2,000 ya kiingilia waliyotoa.
“Sasa ndugu zangu, nawaambia ukweli hadi sasa mmesha tumia sh 200 tu ya kiingilio chezu,..sasa nawapa show ya Sh 1,800 iliyobaki,” alijigamba Roma ambaye muda wote alikuwa akishangilia na ndipo alipomaliza kwa kuimba Wimbo wa Mathematic uliompa tuzo.
Wasanii wengine waliopanda jukwaani hii leo ni pamoja na Ben Pol, AT, Ali Kiba , Barnaba, Omy Dimpoz  na Suma Lee nao wamefunika vibaya katika Tamasha la Kili Music Award Winners Tour lililofanyika katika Uwanja wa sokoine Mjini Mbeya.
Alianza jukwaani kupanda mshindi wa Tuzo ya wimbo Bora wa R&B.
Msanii Ben Paul ambaye alijinyakulia tuzo hiyo kupitia kibao Number One ambapo nae alishambulia jukwaa na kuwaamsha watu kuwa sasa show imeanza.
Alifuata jukwaani Suma Lee ambaye aliongozwa na show kali kutoka kwa vijana wake wane wakike na wakiume na kushangiliwa vilivyo kwa mkongwe huyo wa Bongo Fleva.
Baada ya Ben Pol, alipanda mkali kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi wa Tuzo Wimbo Bora wenye Vionjo vya Kiasili AT na kutoa burudani ya nguvu na  wimbo wa  Vifuu Utundu amabao ulimpa tuzo aliucheza vilivyo na wanenguaji wake wawili wa kike.
Ika fika zamu ya Omy Dimpoz jukwaani kwa kuimba nyimbo yake mpya aambayo alitaraji kuizindua jana katika Ukumbi wa Club Bilicanas jijini Dar es Salaam, single ya Baadae kasha  ile iliyo mpa tuzo ya Wimbo bora wa Kushirikishwa ya Nai Nai aliyo anza kuimba pekeyake na baade kuurudia wimbo huo akiwa na Ali Kiba.
Ali Kiba alibaki jukwaani hapo kama ilivyokuwa mjini Moshi na vijana wake kumfuata kutoa shukrani zao za kupata kura zilizo wapa ushindi wa tuzo ya Wimbo bora wa Zouk Rhumba kupitia wimbo wa Dushelele.
Wakati mara zote pazia la utoaji burudani kwa washindi hao wa tuzo za Kili Music Award 2012 wanaofanya ziara limekuwa likifunga na Roma Mkatoliki leo akapnda wapili kutoka mwisho.
Roma ambaye ni Mshindi wa tuzo mbili za Wimbo Bora wa Hip Hop kupitia wimbo wake wa Mathematics na Tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop, alishambulia jukwaa huku viitikio vyake vikiimbwa na DJ Choka na hata alipomaliza show yake bado mashabiki walimtaka aendelee.
Mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji bora wa Kiume, Barnaba ndiye aliyefunga pazia hilo kwa siku ya leo mjini Mbeya kwa kuimba  ikiwapo inayovuma kwa sasa ya Magube Gube.
Wasanii hao wiki ijayo wanataraji kutoa burudani kama hiyo jijini Mjini Mtwara na tayari walisha tumbuiza na kuwashukuru mashabiki wao wa Mkoani Dodoma na Jijini Mwanza na Moshi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...