Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 30, 2012

DIAMOND KUTUMBUIZA KATIKA SHINDANO LA MISS CHANG'OMBE


Baada ya  kufanya  show ya Big Brother  Afrika Kusini MSANII Abdul Naasib ‘Diamond’ni mmoja wa wasanii watakaotoa burudani kamambe kulipamba  shindano la Redd’s Miss Chang’ombe 2012 shindano litakalofanyika Juni 9 mwaka huu  katika ukumbi wa Quality Centre barabara ya Nyerere Jijini Dar es Slaam.
Wengine watakaopamba shindano hilo la aina yake ni  kundi la Original Commedy akina Joti na bendi ya mapacha watatu ambayo kwa sasa imekuwa moja ya bendi zinayokonga  nyoyo za mashabiki wengi wa muziki hapa nchini.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam msemaji wa Kampuni ya King Promoters  ambao ndiyo waandaaji wa shindano hilo Martin Mauya ameaema kuwa kwa sasa warembo hao wameendelea kufanya mazoezi katika viwanja vya klabu ya TCC Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.
Shindano hilo linatarajia kushirikisha warembo bomba 14 watakaopanda jukwaani kuchuana vikali kumpata mrembo wa mkoa huo wa kimashindano wa Chang’ombe huku baadhi ya wadau wa fani hiyo ya urembo nchini wakitabiri kuwa mrembo wa Tanzania mara hii atatokea katika mkoa huo wa kimashindano.
Mauya  amewataja warembo wanaotarajia kupanda jukwaani ni Elizabeth Mushi, Restituta Faustine, Miriam Ntakisivya, Flora Kazungu, Flora Robert,  Like Abraham, Clara Diu, Margareth Gerald, Jesca Haule, Deborah Nyakisinda, Suzan Paul, Wensley Matius, Zulfa Bundara na Catherine Masumbigana.
‘Kwa sasa warembo hao wanafanya mazoezi na kurudi nyumbani lakini Juni 3 warembo hao wataingia rasmi kambini katika Hoteli moja kubwa Jijini kabla ya kuapnda hiyo Juni 9’ alisema Mauya.
Shindano hilo limedhaminiwa na REDD’S ORIGINAL, NEXUS CONSULTING AGENCY, DODOMA WINE, CXC AFRIKA, PAPAZII INTERTAINMENT, KITWE GENERAL TRADERS,CHERISH, BEN EXPEDITION, SCREEN MASTERS, ARDHI PLAN LIMITED.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...