Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, May 21, 2012

FLAVIANA MATATA KUTOA MSAADA KUMBUKUMBU YA MV BUKOBAMke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal (kushoto) akiwa na Flaviana Matata, katika  hafla iliyofanyika jijini Dar jana. 
Mwanamitindo wa Kimataifa,  Flaviana Matata amekuja nchini akitokea nchini Marekani anakoishi na kufanya shughuli zake, amewasili nchini kwa lengo la kutoa msaada wa Vifaa vya kuokolea maisha Majini (Life Vest) ambavyo atavikabidhi Jijini Mwanza leo.

Ikiwa ni miaka 16 tangu alipompoteza mama yake mzazi katika ajali hiyo ya MV BUKOBA iliyozama katika Ziwa Victoria, Matata ameamua kutoa msaada huo wa vifaa vya kuokolea maisha ikiwa ni sehemu ya kumuenzi na kumkumbuka mama yake mzazi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...