Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 25, 2012

WANAUME FAMILY KUMPA TAFU DOGO ASLAY DODOMA


KUNDI zima la TMK Wanaume Family la Temeke jijini Dar es Salaam, litasindikiza utambulisho wa msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya nchini Aslahi Isihaka ‘Dogo Aslay’ litakalofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma na ukumbi wa Royal Village mjini humo.
Wanaume Family
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana mratibu wa onesho hilo Jackline Masano wa Kampuni ya Ruhazi Promotion ya jijini Dar es Salaam, alisema kuwa TMK Family watafanya vituo vyao kwenye onesho hilo litakalofanyika Jumamosi Juni 9,2012 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Alisema TMK Family wanaungana na wasanii kutoka kituo cha Mkubwa na Wanawe cha Temeke Sandali jijini katika kumsindikiza msanii huyo aliye gumzo hivi sasa kutona na wimbo wake ‘Naenda Kusema’.
“Tunapenda kuwaambia wapenzi wa muziki wa mjini Dodoma na maeneo jirani kwamba Kampuni ya Ruhazi Promotion imekubaliana na TMK Family hivyo mchana wa Jumamosi Juni 09, 2012 kuanzia saa 6:00 mpaka saa 12:00 jioni itakuwa kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma na litaanza saa 2:00 usiku hadi saa 6:30 usiku kwenye ukumbi wa Royal Village,” alisema Jackline Masano.
Alisema pamoja na kwamba onesho hilo litapambwa na wasanii wengi lakini kiingilio kitakuwa shilingi 5,000 tu kwa wakubwa na shilingi 1,000 kwa watoto ili kuwawezesha wapenzi wengi zaidi kukimudu ambapo watapata burudani ya uhakika.
Aliongeza kwamba hivi sasa, wanaendeelea kufanya mazungumzo na wasanii wengine watakaopamba maonesho hayo yote na kwamba pindi mazungumzo yatakapokamilika watawaweka hadharani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...