Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 23, 2012

LULU, KOMBA MAMBO HADHARANI

 
Stori: Mwandishi Wetu/ Chanzo:http://www.globalpublishers.info
HATIMAYE siri ya madai kuwa Mheshimiwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Damian Komba na msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni wapenzi, sasa mambo hadharani, Risasi Mchanganyiko linakupa ukweli.

Mambo hayo ambayo yamekuwa katika vinywa vya watu na kuzagaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwa muda mrefu, yamewekwa kweupe na Mheshimiwa Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa la Tanzania One Theatre (TOT).

LAIVU ITV
Akizungumza katika Kipindi cha Shamsham za Pwani kinachoongozwa na Mtangazaji Hawa Hassan kupitia Runinga ya ITV Jumamosi iliyopita, Kepteni Komba alifunguka kuwa hajawahi kutembea na msanii huyo kama watu wanavyodai.

HUYU HAPA KEPTENI KOMBA

“Huwa ninawasaidia wasanii wa jinsi zote lakini watu wakiona nimemsadia msanii wa kike, wanavumisha kwamba nimemtafuna,” alisema Kepteni Komba.

Alikiri kuwa alishawahi kumpa Lulu gari lake la kifahari pale msanii huyo alipokwenda na marehemu Steven Kanumba kumuomba kwa ajili ya kumpokea mgeni wao, staa wa filamu za Kinigeria, Ramsey Nouah alipotia maguu Bongo miezi kadhaa iliyopita.

“Siyo yeye peke yake, hata JB (Jacob Steven), Ray (Vincent Kigosi) na Kanumba wameshafika kuniomba hata nyumba yangu kufanyia maigizo nikawapa lakini ninapomsaidia JB hawasemi kwa kuwa ni mwanaume, ila nikimsaidia msanii wa kike, watu (wambeya) wanasema nimemtafuna,” alisema Komba kwa mshangao.
LA ROHONI
Mbunge huyo alilazimka kutoa yake ya moyoni baada ya kipindi hicho kufika kwenye kipengele kinachoitwa La Rohoni ambacho humtaka mgeni mwalikwa kusema linalomkereketa moyoni mwake.

“Kwa kweli wanaoendelea kusema, acha waseme lakini ukweli ndiyo huo sihusiki kabisa na habari hizo kwa kuwa siyo za kweli,” aliendelea kufunguka Kapteni huyo mstaafu wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ).
TUMEFIKAJE HAPA?
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai mitaani na mitandaoni kuwa Kepteni Komba ana uhusiano usiofaa na Lulu lakini kwa kauli hiyo mheshimiwa huyo amemaliza utata huo.

Wakati hayo yakijiri, Lulu bado yupo nyuma ya nondo za mahabusu kwenye Gereza la Segerea jijini Dar kwa kuhusishwa na kifo cha Kanumba ambapo kesi yake itafikishwa Mahakama Kuu Mei 28, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...