Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 23, 2012

KAMATI YA MISS TANZANIA YATEMBELEA MAZOEZI YA MISS KURASINI


Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega akiongea na warembo wanaoshiriki katika shindano la Miss Kurasini hawapo pichani ,wakati wa mazoezi yao yanayofanyika kwenye ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa Azizi Ali jijini Dar es salaam, Shindano la kumsaka malkia wa kitongoji hicho linatarajiwa kufanyika siku yajumamosi katika ukumbi huohuo.


Pichani kutoka kulia ni Benny Kisaka mwanadaaji wa Miss Temeke, Albert Makoye mkuu wa Itifaki Miss Tanzania, Bosco Majaliwa Katibu Mkuu Miss Tanzania na nyuma ni Juma Mabakila mwandaaji Miss Ilala
Warembo wanaoshiriki katika shindano la Miss Kurasini wakimsikiliza Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega wakati wa mazoezi ya shindano la Miss Kurasini kwenye ukumbi wa Equator Grill leo jioni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...