Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, May 21, 2012

SBL WAZIBEBA TUZO ZA TASWA SI KITOTO


Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya SBL, Teddy Mapunda akizungumza na Waandishi wa Habari, City Sports Lounge asubuhi ya leo. Wengine kulia ni Katibu Mkuu wa TASWA Amir Mhando na katikati ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto
SOURCE: FULL SHANGWE
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL), imetangaza rasmi kudhamini kwa kitita cha Sh. Milioni 150, tuzo za Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), hafla ambayo inatarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.
Tukio hilo la kihistoria litafanyika katika ukumbi maarufu hapa jijini Dar es Salaam Diamond Jubilee tarehe 14/06/2012 ambapo zaidi ya wageni 500 wanatarajiwa kufurika kushuhudia tukio hilo.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dar es salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda, amesema maamuzi ya kudhamini tukio hilo kwa mara nyingine ni kuendelea kusaidia kuinua michezo nchini. 
“Kufanya hivi ni sehemu mojawapo ya kuwatambua wanamichezo, lakini pia kupitia udhamini huu, tungependa kuwasaidia waandishi wa michezo kujaribu kuangalia ndani zaidi na kuleta mwanga na uelewa wa haraka kwa jamii juu ya michezo mbalimbali iliyopo hasa hapa kwetu Tanzania”alisema Mapunda.
Udhamini huu utatumika katika maeneo mbalimbali kufanikisha sherehe hiyo kama vile chakula cha jioni, burudani,tuzo, vyeti, zawadi pamoja na mahitaji na matumizi mengine ili zoezi hili liwe nzuri na la kukumbukwa nchini”, aliongeza Bi. Mapunda.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kampuni ya bia ya Serengeti inajivunia kuwa mdhamini mkuu wa tuzohizi kwa mwaka wa tatu sasa. “sisi kamaSBL kwakweli tunajivunia kuwa wadau wa tukio hili kwa mara nyingine, lakini pia tunajivunia kuwa na waandishi bora wahabari za michezo ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuinua na kuendeleza tasnia ya michezo hapa nchini kupitia taarifa sahihi zenye kuelimisha jamii juu ya swala zima la michezo” .
SBL imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo hya michezo Tanzania na kwa sababu hiyo, inachukuliwa kama kampuni mfano wa kuigwa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...