Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, April 18, 2011

*AKUTWA HOI AKIUCHAPA USINGIZI KATIKA DIMBWA LA MATOPE SINZA DARAJANI


Wananchi wakazi wa Sinza Darajani Kata ya Sinza D jijini Dar es Salaam, wakimuangalia kijana ambaye hakuweza kufahamika jina lake, aliyekutwa amelala kwenye uwanja wa mpira wa Darajani leo asubuhi huku akiwa bado anapumua.

Baada ya kufika eneo hilo wakazi hao waliweza kusikia sauti ya kijana huyo akiomba msaada wa kupewa maji ya kunywa na alipoulizwa sababu za kuwa katika hali hiyo huku akiwa na majeraha kibao na akiwa amelala katika matope alijibu kuwa alitoka kuiba maeneo ya Tandale na ndiko alipopewa kipigo cha mbwa mwizi na kufanikiwa kutimka ili kujiokoa na alipofika maeneo hayo alizidiwa na kuwanguka, lakini baada tu ya kutoa jibu hlo hakuweza tena kuzungumza wala kufumbua macho hadi Sufianimafoto anatoka eneo hilo.
na www.sufianimafoto.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...