Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, April 30, 2011

WAFANYAKAZI IDARA YA HABARI (MAELEZO) WAMUAGA RASMI MKURUGENZI CLEMENT MSHANA ALIYETEULIWA KUONGOZA TBC

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Clement Mshana (kushoto) akikabidhiwa zawadi iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Idara hiyo na Ofisa Habari Mwandamizi, Anna Itenda (kulia)wakati wa hafla fupi ya kumuaga rasmi iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Mshana ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) .
Clement Mshana, akizungumza na wafanyakazi wa Idara hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na wafanyakazi hao.

Wafanyakazi wa Idara ya Habari (MAELEZO) wakiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo Clement Mshana (katikati) baada ya hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Idara hiyo jijini Dar es Salaam leo mchana. Picha Zote na Aron Msigwa-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...