Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, April 12, 2011

EXIM BANK YAONGEZA PATO


BENKI ya Exim Tanzania imeongeza faida ya pato lake kufikia sh. bilioni 16.6/-hadi mwishoni mwa mwaka jana ikiwa ni ongezeko la 66.7% ukilinganisha na pato la sh. bilioni 9.99 la mwaka wa fedha 2009.


Mafanikio hayo yanaifanya benki hiyo kuwa kinara wa ongezeko la faida katikasekta ya kibenki nchini inayoonyesha kukua kwa kasi katika ufanisi na ubunifukatika utendaji wake.Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na benki hiyo jana nakusainiwa na Meneja Mkuu Dinesh Arora, hatua hiyo ya maendeleo ya kasi inatokanana ushirikiano mzuri kiutendaji uliojengekana miongoni mwa wadau wa benki hiyo.


“Tumeongeza pato letu kwa 66.7% na kufika sh. bilioni 16.6 hadi ilipofikiamwishoni mwa mwaka jana kutoka sh. bilioni 9.99 za mwaka 2009, hivyo ni hatua yakupongezwa”, ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.


Taarifa hiyo inaeleza faida ya uendeshaji wa benki kwa mwaka wa fedha 2010imeongezeka kwa asilimia 60% na kufikia shilingi 23.22 bilioni dhidi ya shilingibilioni 13.87 ukitoa pato la ziada la shilingi bilioni 4 lililopatikana mwishomwa mwaka 2009.Inafafanua kuwa pato la benki kwa ujumla limeongezeka kutoka sh.bilioni 127 nakufikia sh. bilioni 710 ilipofika mwishoni mwa Desemba 2010 na kuifanya Benki yaExim kuwa miongoni mwa benki 6 kubwa nchini kuwa na rekodi nzuri katika pato lajumla.Katika gawio la ‘gross NPA ratio’ benki ya exim imeshuka kufikia 4.1% ilipofikaDesemba 2010 kutoka 4.3% ya Desemba 2009.


Katika kuendelea mbele, Benki ya Eximimeweka kipaumbele kwenye uongozi wa NPA na kufanya tathimini ya kila marakatika kuhakikisha kitengo hicho kinapanda kiubora.“Tumeonekana kushuka kidogo katika sehemu ya NPA lakini benki inafanya jitihadaza makusudi kuhakikisha kuwa mikakati mipya ya kusaidia kuinuka kwa kitengohicho inawekwa”, inasisitiza sehemu ya taarifa hiyo.Benki ya Exim Tanzania ina matawi 22 katika sehemu mbalimbali za nchi ikiwa nipamoja na kuwa na uendeshaji wa kibenki katika Visiwa vya Comoro zinazoongozwana huduma ya ATM ambapo Tanzania zipo 45 na 25 nje ya Tanzania. Katika kuhakikisha benki hiyo inaongeza ufanisi wake kiutendaji, mwaka janaimeajiri wafanyakazi wengine 150 wakiwemo wataalamu watatu kutoka nje ya nchiikiwa ni kuendelea kuonyesha mfano kwa kuwavutia watanzania waishio nje, kurudinyumbani na kufanyakazi.


1 comment:

  1. If you and your Pardner are struggling with marriage counseling, dazed and they aren't masochists. Pic by Jason Kempin/Getty ImagesSinger Katy Perry arrives at The 53rd you are in difficulty, you may go for counseling.

    Feel free to visit my web blog; marriage counseling mn
    my site: relate counselling

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...