Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 28, 2011

CREDO MWAIPOPO AJINADI BONGO
KIUNGO wa zamani wa timu ya soka ya Yanga, Credo Duncan Mwaipopo (pichani kushoto), kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam akisaka timu ya kujiunga nayo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Credo aliyekuwa akicheza soka ya kulipwa nchini Sweden alisema kuwa mkataba wake wa kucheza soka nchini humo umeshamalizika, hivyo yupo tayari kujiunga na timu yoyote itakayomhitaji.
“Nina miezi minne tangu nitue hapa nchini, nipo katika kusaka timu yoyote ya kuichezea hapa nchini na hadi sasa sijapata timu yoyote, hivyo nipo tayari kujiunga na timu yoyote itakayonihitaji,” alisema Credo.
Credo aliyeichezea Yanga kwa mafanikio miaka ya nyuma kabla ya kutimkia nchini Sweden, alieleza kuwa alishindwa kuendelea na klabu yake ya Pannelinois IF inayoshiriki ligi daraja la pili kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimwandama.
Alisema kuwa anaendelea na mazoezi katika viwanja mbalimbali jijini Dar es Salaam ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuonyesha uwezo wake endapo atapata timu itakayomsajili kwa msimu ujao wa ligi.
http://mamapipiro.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...