Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 21, 2011

EXTRA BONGO KUZINDUA TOVUTI SIKUKUU YA PASAKA


Na Addolph Bruno

BENDI ya muziki ya Extra Bongo 'Next Level' inatarajia kuzindua tovuti itakayokuwa ikionesha ikitoa habari na matukio ya bendi hiyo mara baada ya sikukuu ya Pasaka katika ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na majira kwa simu jana, akiwa safarini kutoka Morogoro kwenda jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Ali Choki alisema uzinduzi huo pia utafanyika sambamba na siku ya wasafi.

Alisema tovuti hiyo inazinduliwa maalumu kwa ajili ya kutoa taarifa mbalimbali za bendi ambapo itasindikizwa na burudani ya kukata na shoka ambapo kiingilio kitakuwa ni kwa wanaume ambapo wanawake wataingia bure.

Mbali na hilo Choki alisema katika kusherekea sikukuu ya pasaka bendi hiyo itafanya onesho katika ukumbi wa Dar West, Tabata ambapo kutakuwa na utambulisho wa wimbo mpya wa Rogert Hega uitwao 'Fisadi wa mapenzi' na staili mpya ya uchezaji ya mwanamuziki Hassan Mussa 'Nyamwela.'

"Katika kuhakikisha pia tunatoa burudani kwa mashabiki wetu wote tumepanga kufanya onesho lingine kubwa kwa wakazi wa Morogoro siku ya Mei Mosi katika Hotelya Savoi Inn na hapa ninatoka huko kuweka mambo sawa.," alisema Choki.

Alisema bendi hiyo itaanza kutoa burudani ya pasaka kwa onesho moja la mkesha kwa mashabiki wao katika ufukwe wa Coco ambapo aliongeza safu ya uimbaji na uchezaji wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa burudani safi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...