Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, April 12, 2011

MSONDO NGOMA KUTUMBUIZA DDC KARIAKOO KILA JUMAPILI


BENDI Kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' inatarajia kuanza kufanya onesho kila jumapili katika ukumbi wa DDC Kariakoo badala ya ukumbi wa Max bar Ilala kupanua wigo wa burudani kwa mashabiki wake.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema hatua hiyo imefikiwa kutokana na maombi mengi ya mashabiki wao wa maeneo hayo.

"Maombi yao yalitokana na ukumbi huo kuwa mdogo na sisi tukaona ni vyema kuwasikiliza kwa sababu muziki ni mashabiki na bila wao sisi sio kitu kwa pamoja tumeafiki sasa wakazi wa Dar es Salaam Msondo Tupo DDC Kariakoo kila Jumapili kwa burudani zaidi.," alisema Super D

Alisema wataanza kufanya onesho lao la kwanza katika ukumbi huo Jumapili hii ambapo kutakuwa na burudani kabambe kutoka kwa wanamuziki wao akiwemo Shaaban Dede aliyejiunga nao hivi karibuni akitokea Sikinde.

Alisema siku hiyo kutakuwa na utambulisho wa nyimbo zao mpya mbili kwa mara ya kwanza ambazo ni Suruhu ulioimbwa na Dede na mwingine mmoja ambao haujapewa jina ulioimbwa na Hassan Moshi 'Tx Junior'.

Alisema wanawaomba wapenzi wao wanaoishi maeneo ya kariakoo, Ilala na maeneo ya jirani kujitokeza katika ukumbi huo ambao awali ulikuwa ukitumiwa na mahasimu wao Mlimani Park 'Sikinde'. ambapo kila jumamosi wanatumbuiza katika ukumbi wa Sigara uliopo Chan'gombe

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...