Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, April 30, 2011

MAPACHA WATATU NA WANAUME TMK KUTUMBUIZA IKWETA GRILL LEO


BENDI ya muziki wa Dansi ya Mapacha Watatu na Kundi la muziki wa kizazi kipya TMK Wanaume Family, leo watafanya onesho moja kwenye Ukumbi wa Ikweta Grill uliopo Mtoni kwa Azizi Ali, Temeke.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa onesho hilo, Zahor Said alisema kuwa maandalizi ya onesho hilo yamekamilika kama walivyopanga na wapenzi wote wa burudani katika sehemu za Temeke na maeneo ya jirani watarajie mambo makubwa.
Alisema katika onesho hilo litakaloanza saa 3 usiku, watoto wa Temeke, Wanaume Family watakuwa wa kwanza kufanya makamuzi yao juu ya jukwaa ikiwa ni mara yao ya kwanza kufanya onesho kwenye ukumbi huo.
Said alisema mapacha wao watatoa burudani yao ikiwa ni pamoja na kupeleka tuzo zao za Kili Music Awards ambazo walizitwaa kutokana na umahiri wao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...